#HABARI: Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha na Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Cecilia Daniel Paresso, ametoa msaada wa mbao zenye thamani ya shilingi milioni mbili na laki tano kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi wa CCM Wilaya ya Karatu.
Mbao hizo zimekabidhiwa leo mbele ya viongozi na wanachama, ikiwa ni sehemu ya mchango wake wa awali katika kuboresha mazingira ya makazi ya watumishi wa chama hicho.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Mhe. Paresso amesisitiza umuhimu wa mshikamano katika kuimarisha miundombinu inayowawezesha watumishi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Amesema kuwa ushirikiano huo ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha chama kinakuwa na mazingira bora ya kazi yanayochochea maendeleo ya ndani na utumishi uliotukuka kwa wananchi.
Kwa upande wao, viongozi wa CCM Wilaya ya Karatu wamemshukuru Mhe. Paresso kwa mchango huo ambao utakuwa chachu ya kuharakisha ujenzi wa nyumba hizo.
Wamebainisha kuwa msaada huo ni mfano wa kuigwa na unatoa hamasa kwa wadau wengine kujitokeza kuchangia mradi huo ili uweze kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.