#HABARI: Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imekagua Kituo cha Kupokea na Kupoza Umeme cha Mpomvu mkoani Geita leo Machi 15, 2026, ili kuona maendeleo ya miradi ya kimkakati.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Subira Mgallu, ameeleza kuridhishwa na uwekezaji wa shilingi bilioni 50 katika kituo hicho ambacho kina uwezo wa kusambaza megawati 90, kikiwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi na shughuli za kiuchumi.
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amebainisha kuwa kituo hicho kimesaidia kuondoa changamoto ya umeme mkoani Geita, ambapo awali mkoa ulikuwa ukitegemea megawati 4 pekee kutoka Shinyanga.
Kwa sasa, kituo cha Mpomvu hakihudumii Geita pekee, bali kinasambaza nishati katika maeneo ya Biharamulo, Ngara, Sengerema, na Kakonko, kikiimarisha shughuli za kijamii na kiuchumi katika mikoa ya jirani.
Aidha, serikali imeweka mpango wa kuongeza laini maalum kwa ajili ya Mgodi wa GGM, ambao mahitaji yake yanatarajiwa kuongezeka kutoka megawati 36 hadi megawati 70 ifikapo mwaka 2035.
Mradi huu uliozinduliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mwaka 2022, unatajwa kuwa suluhisho la kudumu katika sekta ya madini na ukuaji wa kasi wa viwanda katika Kanda ya Ziwa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.