Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema siku ya Jumamosi, Machi 14, kwamba “njia za kidiplomasia zinawezekana” kukomesha vita kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah wanaounga mkono Iran huko Lebanon, wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Beirut.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika Hoteli ya Phoenicia, karibu na eneo ambapo mamia ya familia zilizohamishwa zimerundikana kwenye mahema ya muda, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kusitisha mapigano kwa dharura, anaripoti mwandishi wetu huko Beirut, Sophie Guignon. “Walebanoni hawakuchagua vita hivi; walingizwa tu ndani yake dhidi ya mapenzi yao. Ujumbe wangu kwa pande zinazopigana uko wazi: komeshani mapigano, acheni kufanya mashambulizi ya mabomu.” “Hakuna suluhisho la kijeshi, diplomasia pekee, mazungumzo pekee,” amesisitiza António Guterres.

“Tunafanya kila linalowezekana ili kufanikisha kupunguza mapigano na kukomesha uhasama mara moja,” ameongeza, akisema kwamba Umoja wa Mataifa “umekuwa ukiwasiliana mara kwa mara na wahusika wote ili kuleta pande zote kwenye meza ya mazungumzo.” Akihutubia jumuiya ya kimataifa, ameongeza: “Imarisheni kujitolea kwenu. Saidieni taifa la Lebanon na vikosi vya jeshi vya Lebanon ili kuhakikisha vina uwezo na rasilimali zinazohitajika.”

Antonio Guterres, ambaye aliwasili Beirut siku iliyotangulia kwa “ziara ya mshikamano,” amekutana Jumamosi na mkuu wa majeshi, Rodolphe Haykal, taasisi ya kijeshi imebainisha. Majadiliano yalilenga hitaji la kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwishoni mwa mwaka 2024 kati ya Israel na Hezbollah, na kuhusu utekelezaji wa jeshi la mpango wake wa kupokonya silaha kundi hili la Washia.

Idadi rasmi ya hivi karibuni kutokana na mashambulizi ya Israel nchini Lebanon, iliyotolewa Jumamosi, inafikia watu 826 waliouawa na zaidi ya 800,000 wameyakimbia makazi yao, huku Israel ikiwataka wakazi wa sehemu kubwa za nchi kuhama. “Ilani za uokoaji zimetolewa wakati idadi kubwa ya watu walio hatarini wakiwa katika maeneo yaliyoathiriwa hazihakikishi usalama wa kutosha kwa raia,” jambo ambalo “bila shaka ni ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu,” mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alisema.

Kituo cha afya kusini mwa Lebanon pia kililengwa na Israel, na kuwaua madaktari na wauguzi 12. Shambulio hili la hivi karibuni dhidi ya wafanyakazi wa afya limesababisha lawama kutoka kwa mamlaka ya Lebanon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *