
Katika siku ya 15 ya vita vya Mashariki ya Kati, Donald Trump ametoa wito kwa nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, kutuma meli kusaidia kulinda Mlango-Bahari wa Hormuz. Moto ulizuka katikati ya Israel kufuatia mashambulizi ya makombora ya Iran usiku wa kuamkia leo Jumapili.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uharibifu wa vifaa umeripotiwa kufuatia moto uliosababishwa na vipande vya makombora katikati ya Israel.
Mwanamume mwenye umri wa miaka 80 amejeruhiwa kidogo na vipande vya kombora, na mwanamke wa umri huo alipata majeraha madogo kutokana na kuvuta moshi katika eneo la tukio huko Holon. Wahudumu wa afya wa Magen David Adom wametoa huduma ya kwanza.
Ving’ora vyasikikaTel Aviv, katikati ya Israel, na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, kulingana na Haaretz
Ving’ora vimesikika katika maeneo mengi ya Israel na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, kulingana na gazeti la Israeli Haaretz, ambalo limeongeza kuwa vipande vya makombora na vimeanguka karibu na Tel Aviv, kulingana na vyanzo vya polisi.
Milipuko mikubwa iyasikika Manama, Bahrain, kulingana na AFP
Milipuko mikubwa imesikika Jumapili usiku huko Manama, mji mkuu wa Bahrain, huku Iran ikiendelea na mashambulizi yake dhidi ya majirani zake wa Ghuba, kulingana na waandishi wa habari wawili wa AFP. Tangu kuanza kwa vita, Bahrain imesema imezuia makombora 125 ya Iran na ndege zisizo na rubani 203 za Iran na inaripoti vifo viwili. Katika nchi zingine za Ghuba, mashambulizi haya yamesababisha vifo 24.
Marekani inaamuru wafanyakazi wasio wa lazima kuondoka Oman kutokana na vita na Iran
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imetangaza kuwa imewaamuru wafanyakazi wasio wa lazima wa serikali na wanafamilia wao kuondoka Oman, ikitaja hatari za kiusalama huku vita kati ya Israel na Marekani na Iran vikiendelea.