Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Jumanne Misungwi, amewaomba Watanzania kuendelea kumuombea Rais ili aweze kuiongoza nchi kwa hekima, busara na mafanikio zaidi kwa manufaa ya wananchi.

Misungwi ametoa wito huo wakati wa hafla ya futari aliyoiandaa kwa waumini wa Kiislamu na wasio waislamu akisema maombi yana mchango mkubwa katika kudumisha amani, mshikamano na maendeleo ya Taifa.

Amesema ni muhimu Watanzania kuendelea kuwa na moyo wa umoja na kushirikiana katika kumuunga mkono Rais katika juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo na kuboresha ustawi wa maisha yao.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza mshikamano, upendo na kuheshimiana.

#startvupdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *