Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imetangaza katika taarifa rasmi kwamba manowari za nchi hiyo hazitashiriki katika operesheni yoyote ya mashambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya habari za kimataifa, Wizara hiyo imeeleza kuwa manowari ya kubeba ndege inayotumia nguvu za nyuklia, Charles de Gaulle, pamoja na kikosi chake cha kivita cha baharini, haitahusika katika hatua zozote za mashambulizi dhidi ya Iran.

Taarifa hiyo, iliyotolewa siku ya Jumapili, imesisitiza kuwa: “Kikosi cha manowari cha Charles de Gaulle hakina jukumu lolote la kushambulia, wala hakitashiriki katika operesheni za mabomu au mashambulizi dhidi ya ardhi ya Iran. Msimamo wa Ufaransa ni wa kujilinda tu, ukiwa na lengo la kupunguza mvutano na kulinda uhuru wa usafiri wa majini, si kuchochea au kupanua mzozo.”

Rais wa Marekani juzi alitoa ombi kwa nchi waitifaki kama vile Ufaransa, Uingereza na Japan kujiunga na vita dhidi ya Iran kwa kutuma meli zao za kivita katika Ghuba ya Uajemi.  Awali Trump alidai kwa kiburi kuwa jeshi la mjini la Marekani linaweza kukabiliana na Iran peke yake lakini sasa inaonekana hilo haliwezekani. Hakuna nchi yoyote iliyokubali mwito wa Trump wa kujiunga na vita ilivyoanzisha dhidi ya Iran kwa kushirikiana na utawala haramu wa Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *