Kiongozi wa upinzani Bobi Wine ametangaza katika video kwamba ameondoka Uganda siku ya Jumamosi, Machi 14. Bobi Wine amekuwa mafichoni tangu uchaguzi wa urais wa mwezi Januari, ambao Yoweri Museveni alishinda, kwa kuchaguliwa tena kwa muhula wa saba. Kiongozi huyo wa upinzani alilaani matokeo hayo kuwa ya udanganyifu. Bobi Wine anakusudia kuendelea na mapambano yake kutoka nje ya nchi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe wa video uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, Bobi Wine anawahutubia Waganda na kwa mara nyingine tena analaani kitendo cha rais Museveni “kujipa kwa nguvu madaraka baada ya kuminya matakwa ya raia wa Uganda”  wakati wa uchaguzi wa hivi karibuni.

Kiongozi huyo wa upinzani anazungumzia kwa kina kuhusu unyanyasaji aliofanyiwa katika miezi miwili iliyopita: “Utawala umenitafuta kila mahali,” anasema, akiorodhesha msako mwingi na vitendo vya vitisho vilivyotendewa familia yake na marafiki.

Bobi Wine – ambaye amekuwa akiishi mafichoni tangu uchaguzi – ametoa shukrani zake kwa Waganda wote waliomuunga mkono na kumlinda wakati wote huu.

“Inachekesha kwamba wakati wote huu, idara za usalama za Uganda zmewekeza mamilioni ya fedha za umma zikitafuta kila mahali, bila mafanikio,” amesema kwa kejeli.

Katika video hii, Bobi Wine anaonyesha kwamba kuondoka kwake nchini kutakuwa “kwa muda mfupi” na kwamba ataendelea na “kazi” yake nje ya nchi.

“Katika wiki zijazo, nitazungumza na (…) washirika wetu kote ulimwenguni kabla ya kurudi Uganda kuendelea kukuza uhuru na demokrasia,” amesema. Kurudi kwake Uganda kutafanyika “chini ya macho ya ulimwengu.”

“Baada ya yote, sijafanya uhalifu wowote,” Bobi Wine ametangaza, “kugombea urais si uhalifu,” ameongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *