#HABARI: Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, Mhe. Florent Kyombo, ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) kwa usimamizi thabiti wa miradi ya kimkakati ya TACTIC jijini Arusha.
Baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Bondeni City, masoko ya Mrombo na Kilombero, pamoja na bustani ya Themi leo Machi 17, 2026, kamati hiyo imeridhishwa na kiwango bora cha utekelezaji ambacho sasa kinatumika kama mfano kwa miji na majiji mengine 45 nchini yanayotekeleza miradi kama hiyo.
Mhe. Kyombo amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi hiyo na kumpa dhamana Waziri wa Nchi, Prof. Riziki Shemdoe, ambaye amehakikisha maoni ya wadau yanazingatiwa kama sharti muhimu la Benki ya Dunia.
Kwa upande wao, wajumbe wa kamati hiyo wakiongozwa na Mhe. Jafari Chege na Mhe. Hawa Mwaifunga, wameeleza kufarijika na hatua ya ujenzi wa kituo hicho cha mabasi ambacho kitakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi.
Diwani wa Kata ya Themi, Mhe. Melance Kinabo, ameshukuru kwa niaba ya wananchi akibainisha kuwa kukamilika kwa miradi hiyo minne kutaongeza fursa za ajira na kutanua wigo wa kipato kwa wakazi wa Arusha.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.