Nchini Togo, mamlaka zimekuwa zikichunguza, katika wiki za hivi karibuni, visa vinavyotia wasiwasi vya watu wanaotoweka, hasa vijana. Kesi hizi ziliripotiwa kwenye mitandao ya kijamii, kulingana na serikali ya Togo, ambayo imeunda tume maalum ya kutoa mwanga kuhusu masuala haya. Matokeo ya uchunguzi yaliwasilishwa wiki iliyopita kwa Baraza la Mawaziri na kisha kwa vyombo vya habari na wanachama wanne wa serikali.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kwa raia ya Togo katika wiki za hivi karibuni, kwenye mitandao ya kijamii. Visa vinavyotia wasiwasi vya watu wanaotoweka, hasa vijana, vimeshirikiwa, vikiambatana na picha, majina, na mazigira ya kutoweka kwao. Mwishoni mwa mwezi Januari 2026, mamlaka ya Togo iliamua kukabiliana na suala hilo, ikianzisha tume ya uchunguzi na nambari ya simu isiyolipishwa, 1014, kuripoti hali zinazotiliwa shaka.

Jumla ya kesi 102

Kulingana na mawaziri waliotoa taarifa mpya, hakuna ushahidi uliopatikana kuthibitisha kuwepo kwa mtandao wa uhalifu uliopangwa unaohusika na utekaji nyara. Jumla ya visa 102 vimeripotiwa, hasa katika Greater Lome. Kati ya visa hivi 102, watu 86 wamepatikana, wakiwemo watoto 63. Kulingana na mamlaka, visa vingi vinahusiana na kutoroka au kuondoka kwa hiari. Hata hivyo, kesi moja inayoshukiwa kuwa ya utekaji nyara inachunguzwa kwa kina. Na watu 16 bado hawajulikani walipo.

Matumizi ya mitandao ya kijamii kwa uwajibikaji

Mashirika kadhaa ya haki za binadamu ya Togo ambayo tuliwasiliana nayo yalisema kwamba hayajapokea ripoti za aina hii ya kesi hivi karibuni. Huku yakitoa wito wa matumizi ya mitandao ya kijamii kwa uwajibikaji, serikali ya Togo ilielezea hatua zilizochukuliwa: hifadhidata ya kitaifa ya watu walioyoweka, kuimarisha doria na ufuatiliaji wa wimbi la wahamiaji, pamoja na kampeni za uhamasishaji kuhusu hatari za ahadi za pesa rahisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *