Watu zaidi ya 400 wamefariki dunia  na wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya kituo cha afya kushambuliwa nchini Afghanistan, katika tukio linalodaiwa kuhusisha mashambulizi kutoka Pakistan.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ya Afghanistan, Zabihullah Mujahid, kupitia mtandao wa X, amelaani vikali shambulio hilo lililotokea siku ya Jumatatu, akilitaja kuwa ni la kinyama na linalokiuka haki za binadamu.

Pakistan imekuwa ikifanya mashambulizi nchini Afghanistan, hasa karibu na mji wa Kabul, ikidai kuwa serikali ya Afghanistan inatoa hifadhi kwa wanamgambo wanaotishia usalama wake.

Uharibifu uliosababishwa na shambulio la Pakistan jijini Kabuli
Uharibifu uliosababishwa na shambulio la Pakistan jijini Kabuli REUTERS – Sayed Hassib

Mapigano kati ya Afghanistan na Pakistan yalianza mwezi Oktoba mwaka jana. Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa watu 75 walifariki dunia mwezi Februari mwaka huu nchini Afghanistan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *