DAR ES SALAAM: wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na kuimarisha mshikamano bila kujali tofauti za kidini zilizopo kati yao ili kujenga taifa la kesho lilio bora.

Chalamila ameeleza hayo Machi 17 Dar es Salaam katika hafla ya Iftari iliyokutanisha watu wa makundi mbalimbali yenye uhitaji wakiwemo watoto yatima, wanaoishi katika mazingira magumu na watu wasioona, iliyoandaliwa na Ikhsan Aid Network na GSM.

Akizungumza katika hafla hiyo, Chalamila amesema ni muhimu kwa Watanzania kuendelea kushikamana, kupendana na kuishi kwa amani na ushirikiano, si tu wakati wa mwezi wa Ramadhan bali kila wakati.

“Ni muhimu kuendeleza utamaduni wa kupendana na kusaidiana bila kujali dini zetu, kwani sisi sote ni Watanzania,” amesema Chalamila.

Ameeleza kuwa matukio kama ya Iftar yana nafasi kubwa ya kuwakutanisha watu wa dini tofauti na kujenga uelewano, jambo linalochangia kudumisha amani na utulivu wa nchi, akiisitiza Ramadhan ni zaidi ya ibada.

Kiongozi wa taasisi ya Ikhsan, Mussa Omary amesema taasisi hiyo imeanzishwa hivi karibuni ikihusisha muunganiko wa vijana takriban 35 waliosukumwa kuunga mkono makundi yenye uhitaji wakiwemo watoto yatima, wanaoishi katika mazingira mahumu na watu wenye mahitaji maalumu.

“makundi ya yenye uhitaji yapo mengi lakini na makundi ya kutoa msaada pia yapo mengi kama sisi leo hapa tumeshirikiana na GSM na Stateoil ili kuweza kuwasaidia na wanachokifanya kama taasisi ni kuhakikisha wanakuwa na majina ya vikundi vyote vyenye uhitaji ili wajue namna wanaweza kuwafikia,” amesema Omary.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *