Uongozi wa Young Africans Sports Club umefikia uamuzi wa kumuongeza kwenye benchi la Ufundi, Kocha Abdihamid Moalin kama Kocha Msaidizi wa Kocha Pedro Goncalves.

Kocha Moalin amewahi kuhudumu katika Klabu hiyo kama Mkurugenzi wa Ufundi na Kocha Msaidizi katika vipindi tofauti chini ya Kocha Sead Ramovic na Miloud Hamdi na kupata mafanikio makubwa ya kushinda Kombe la Ligi Kuu 2024/2025, Kombe la Shirikisho la CRDB 2025na Kombe la Muungano 2025.

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *