Sera mpya iliyopanuliwa na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump, huenda ikawafanya wasafiri kutoka nchi tano za Afrika zilizofuzu Kombe la Dunia la mwaka huu kuweka dhamana ya hadi dola elfu 15 ili kuingia Marekani kwa ajili ya mashindano hayo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa sera hii, mashabiki toka kwenye nchi hizo watalazimika kulipa kwanza kiasi hicho cha fedha kama dhamana na viza ya kuruhusiwa kuingia Marekani na kisha kurejeshewa baada ya kuwa umeondoka kwenye taifa hilo.

Mpango huu wa majaribio ulitangazwa mwaka 2025 na ulizilenga nchi za bara la Afrika, mashariki ya Kati, Latini Amerika na baadhi kutoka ukanda wa Asia, wiki iliyopita wizara ya mambo ya nje ikitaja orodha mpya yan chi 50 ambazo raia wake watatakiwa kuweka dhamana hiyo.

Chini ya utaratibu huu raia wa Algeria, Cape Verde, Ivory Coast, Senegal na Tunisia ambazo zote zimefuzu kucheza fainali za kombe la dunia la mwaka huu, mashabiki wao watalazimika kwanza kulipa fedha hiyo kabla ya kupewa viza.

Kuelekea fainali hizi zitakazochezwa kwenye nchi ya Marekani, Mexico na Canada, kumekuwa na wasiwasi kuhusu ubaguzi wa mashabiki toka katika baadhi ya nchi, wadai wakilitaka shirikisho la soka duniani, FIFA kuiomba Marekani kulegeza makataa hayo.

Michuano hii inatarajiwa kuanza kutumia vumbi kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, ambapo fainali itachezwa Marekani kwenye uwanja wa MetLife huko New Jersey.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *