Mwanaume mmoja mkazi wa Kijiji cha Imalanguzu Mkoa wa Tabora, Bunzali Jidola (30), anadaiwa kumuua mtoto wake mchanga wa miezi miwili kwa kumchinja na kitu chenye ncha kali.
Aidha, mwanaume huyo pia amemjeruhi mkewe Geni Ndaki (24), kisha kujingonga katika nguzo za umeme.
Akisimulia mkasa huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP, Richard Abwao amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi baada ya mtuhumiwa kuhisi mtoto huyo sio wake.
Kwa mujibu wa Kamanda Abwao, mwanaume huyo alitekeleza tukio hilo siku mbili baada ya kurejea kutoka machimbo ya madini ya Bulangamilwa, wilayani Igunga ambapo alikuwa akijishughulisha na uchimbaji wa madini tangu Agosti 8, Mwaka jana.
Kamanda Abwao amesema mara baada ya kutekeleza mauaji hayo ya mtoto huyo na kumjeruhi mkewe, Bunzali alikutwa amejinyonga kwenye nguzo ya umeme ya TANESCO kijijini humo.
Amesema kwa sasa mwanamke huyo anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Nkinga.
#StarTvUpdate
(Feed generated with FetchRSS)