Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt Aneth Komba amefunga rasmi kikao kazi cha siku tatu cha kuandaa maudhui ya Kuhesabu katika “Kalimani App” kwa kutumia mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2023 na Kamusi ya Lugha ya Alama ya Tanzania.

App hiyo inaandaliwa kwa ajili wanafunzi viziwi wa darasa la awali, la kwanza na la Pili.

Akifunga kikao kazi hicho Mkurugenzi Mkuu Dkt Komba amesema, maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 yemejikita katika kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa ni jumuishi na kuwa hakuna mtoto hata mmoja anayeachwe.

“Wazazi wenye watoto wenye mahitaji maaalum naomba muwapeleka shuleni kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imeandaa mazingira wezeshi kwa watoto wote wakiwemo wenye mahitaji maalumu.”amesema Dkt Komba

Ameeleza TET itashirikiana kwa ukaribu na Jenga Hub kuhakikisha kuwa lengo la kuandaa App linafikiwa na kuwa App hii inawanufaisha walengwa wote nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jenga Hub iliyobuni Kalimani App, Nancy Sumari, ameeleza kuwa App hii imelenga kutumiwa na watoto viziwi wa darasa la awali, la Kwanza, pili na la tatu.

Nancy ameishukuru sana TET kwa kuwa tayari kushirikiana na taasisi ya Jenga Hub katika kuhakikisha kuwa watoto viziwi nao wanapata haki yao ya msingi ya kupata vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

#StarTvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *