#HABARI: Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, ametoa wito kwa vijana mkoani humo kuhakikisha wanalinda amani na utulivu wa nchi kwa nguvu zote.
Amesema kuwa aina yoyote ya vurugu, chokochoko, au kelele hazitapewa nafasi ndani ya Mkoa wa Kagera, kwani amani ndiyo msingi mkuu wa maendeleo kwa vijana na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza kwa niaba ya vijana, Faris amesisitiza kuwa wataendelea kulinda hadhi na heshima ya viongozi wa Chama na Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema kuwa vijana wa Kagera wako imara kumuunga mkono katika jitihada zake za kuliletea Taifa maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa katika mkutano wa hadhara wa Katibu wa NEC Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Ndugu Kenani Kihongosi, ikiwa ni sehemu ya ziara na mikutano ya kuimarisha chama na kusikiliza kero za wananchi uliofanyika Kata ya Kasharunga, Wilaya ya Muleba.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)