#HABARI: Wananchi wa kaya 150 za kata za Kibaoni, Michenga, Lumemo na Lipangalala katika Halmashauri ya mji wa Ifakara, Jimbo la Kilombero, mkoani Morogoro, wamelishukuru Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa kuwapatia msaada wa tani kumi za unga, unaolenga angalau kupunguza maumivu, kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha Machi 24 na 25, 2026.

Msaada huo umepokelewa na Mbunge wa jimbo la Kilombero, Mheshimiwa Abubakari Asenga, mbele ya wananchi wa kata hizo katika hafla fupi iliyofanyika Kijiji cha Kbaoni, Kata ya Kibaoni, Halmashauri ya Mji wa Ifakara, mkoani Morogoro.

Akizungumzia msaada huo, Mheshimiwa Asenga, amesema analishuru Shirika la Reli Tanzania, kuwasaidia wananchi wa Ifakara walioathirika na mafuriko hayo a kutoa wito kwa taasisi za umma na binafsi, mashirika kuiga mfano wa TRC.

Awali, Mkuu wa kitengo cha Uhusiano cha TRC, Bw. Fredy Mwanjala, alisema TRC, imeguswa na hali iliyowakumba Watanzania, wa Jimbo la Kilombero kufuatia mafuriko aidha, kwa niaba ya Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TRC na Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Machibya Shiwa, TRC inatoa msaada wa tani 10 za unga zenye thamani ya shilingi milioni 16, angalau kusaidia kupunguza makali ya athari iliyojitokeza.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *