Rais wa Marekani Donald Trump anapanga operesheni ya kijeshi kwa lengo la kuchimba pauni 1,000 za urani nchini Iran, Jarida la Wall Street linaripoti.

Operesheni hiyo “huenda ikaviweka vikosi vya Marekani ndani ya nchi kwa siku kadhaa au zaidi”, kulingana na Jarida hilo, ambalo linawanukuu maafisa wa usalama ambao hawakutajwa.

Trump bado hajafanya uamuzi, lakini “kwa ujumla yuko tayari kutekeleza wazo hilo, kulingana na maafisa, kwa sababu inaweza kusaidia kutimiza lengo lake kuu la kuzuia Iran kutotengeneza silaha ya nyuklia.”

BBC imewasiliana na Ikulu ya White House na Pentagon kwa maoni kuhusiana na taarifa hii.

Gazeti la New York Times linaripoti kwamba wanajeshi waliopelekwa katika eneo hilo “wanaweza kutumika katika operesheni inayolenga madini ya urani ya Iran iliyorutubishwa sana kwenye eneo la nyuklia la Isfahan” lakini pia wanaweza kutumiwa kuteka Kisiwa cha Kharg au kulinda Mlango- Bahari wa Hormuz.

Mwanzoni mwa mwezi huu Gazeti la New York Times liliripoti kwamba Trump “anazingatia” operesheni ya “kukamata na kuharibu nyenzo za nyuklia za kiwango cha chini kabisa zinazoaminika kuhifadhiwa kwa kiasi kikubwa chini ya mlima huko Isfahan”.

Magazeti yote mawili yanaonyesha kuwa operesheni hiyo itakuwa ngumu na hatari zaidi.

#chanzobbcswahil
#Star TvUpdate

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *