#HABARI: Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imewataka wadau wote wa sekta ya usafirishaji nchini, kutopandisha nauli kwa kigezo cha kupanda kwa bei za mafuta na badala yake wafuate utaratibu rasmi utakaowekwa na watakaopandisha hawatasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.
Akitoa kauli hiyo Kibaha mkoani Pwani wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mkuu wa Latra CPA. Dkt. Habibu Suluo, amesema Aprili 8 ndio kitafanyika kikao cha wadau kujadili jambo hilo jijini Dar es Salaam.
Akaongeza kuwa wasafirishaji wanapaswa kujua kuwa hata wananchi bei hizo mpya zinawaumiza na hivyo nao wawe na huruma nao siyo kukimbilia tu kupandisha bei ya nauli.
Mkurugenzi huyo akaongeza kuwa wasafirishaji wote wanaotaka nauli zipande waje na maelezo ya kina namna wanavyotaka ipande na iwe kwa kiasi gani kwa mujibu wa sheria zinavyowataka.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
BajetiBungeni
(Feed generated with FetchRSS)