Aliyekuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25,2025 kupitia Chama Cha NCCR Mageuzi, Dkt Eveline Wilbard ameteuliwa kuwa mbunge wa Viti Maalum.

Dkt Eveline ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho ameteuliwa leo siku moja baada ya Rais Samia kufanya mkutano na waliokuwa wagombea na wagombea wenza wao wa nafasi ya urais Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu imesema kuwa uteuzi huo umeanza mara moja.

Rais Samia amemteua kiongozi huyo kupitia nafasi zake 10 ambako leeo pia amemteua Angela Kizigha aliyekuwa msaidizi wake wa karibu kuwa mbunge wa Viti Maalum.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *