Maadhimoisho ya kumbukumbu ya miaka 32 ya mauaji ya kimbari yaliyofanywa dhidi ya Watutsi yameanza Leo JUmanne Aprili 7, 2026, nchini Rwanda. Kipindi cha siku 100 cha ukumbusho kimezinduliwa ili kuenzi kuwakumbuka wahanga zaidi ya 800,000 wa mauaji ya kimbari ya 1994. Jijini Kigali, Jumanne asubuhi, maadhimisho hayo yalianza katika Ukumbusho wa Kitaifa wa Gisozi, ambapo Rais Paul Kagame amehutubia taifa.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Kigali, Lucie Mouillaud

“Tunakusanyika kukumbuka,” Rais Paul Kagame ametangaza katika hotuba iliyochukua takriban dakika arobaini, akibainisha mshikamano wake na manusura wa mauaji ya kimbari.

Hotuba iliyolenga zaidi kuzuia kauli za chuki, “ambazo zinageuka kuwa vitendo vya chuki,”rais Paul Kagame ameongeza, pia akishutumu kutochukua hatua kwa jumuiya ya kimataifa mwaka 1994: “somo la kikatili” kwa Wanyarwanda, kulingana na rais Paul Kagame.

Ulinzi wa majeshi ya Rwanda

Akijibu vikwazo vya hivi karibuni vya Marekani dhidi ya jeshi la Rwanda na maafisa wake wanne wa ngazi za juu, “hakuna vikwazo au matusi ya nje yanayoweza kuharibu heshima na uadilifu” wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF), rais amebainisha. Ameelezea hatua hizo kuwa zisizo za haki wakati wa hotuba yake.

“Tunachoomba kwa washirika wetu,” almesema, “ni kujiunga nasi katika mapambano dhidi ya ukabila badala ya kuiadhibu Rwanda kwa kujilinda.”

Baada ya sherehe katika Ukumbusho wa Gisozi, ambapo zaidi ya wahanga 250,000 wa mauaji ya kimbari wamezikwa, programu ya maadhimisho ya kumbukumbu inaendelea Aprili 7, kwa maandamano ya kuwakumbuka wahanga na yale yaliyotokea nchini humo na ibada mbalimbali zitakazo anza Jumanne jioni katika uwanja wa BK Arena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *