Mbunge wa Ikungi Magharibi, Elibariki Kingu, ameishauri Serikali kujenga miundombinu ya kuhifadhi mafuta (storage facilities) ili kuhakikisha upatikanaji wa akiba ya kutosha kwa matumizi ya dharura na fursa ya kuuza nje pale inapowezekana.
Kingu ametoa ushauri huo bungeni leo akichangia mjadala wa bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu, akieleza kuwa uwepo wa hifadhi ya mafuta utaisaidia nchi kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya bei na upatikanaji wa nishati, hususan katika kipindi hiki cha mzozo wa vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa Serikali kuchukua hatua za kupunguza gharama zisizo za lazima katika matumizi ya umma, pamoja na kuondoa baadhi ya tozo ili kupunguza mzigo wa bei ya mafuta kwa wananchi.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)