Muongozaji wa Kitaifa wa Miss World Tanzania, Mustafa Hassanali, amesema jumla ya wasichana 20 kutoka mikoa mbalimbali wamechaguliwa kuingia kambini kwa ajili ya mchakato wa kumpata mwakilishi wa Tanzania katika shindano la kimataifa la Miss World.
Ameeleza kuwa lengo la kambi hiyo ni kuwajengea washiriki uwezo na kuchuja mshindi bora atakayeiwakilisha nchi kimataifa na kuipeperusha bendera ya Tanzania. Hassanali amesisitiza kuwa mchakato huo hauzingatii urembo pekee, bali pia unatazama mchango wa mshiriki katika jamii, maadili, kujiamini pamoja na uwezo wa kuwasiliana.
#AzamTVUpdates
✍Ibrahim Kilumbo
Mhariri | John Mbalamwezi
@goodluckpaul_mc @hildaphoya
(Feed generated with FetchRSS)