
MCHEZAJI wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Klabu ya Simba, Abdallah Kibadeni ‘Mputa’, amewataka vijana kote nchini kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali badala ya kujihusisha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani ya nchi.
Kibadeni ameyasema hayo katika mahojiano maalumu, akisisitiza umuhimu wa vijana kutumia vyema nafasi wanazopewa na kushirikiana katika kulinda amani, akibainisha kuwa ustawi wa taifa lolote unategemea uwepo wa amani. Ameongeza kuwa michezo ni daraja muhimu la kuwaunganisha watu, hivyo amewahimiza wanamichezo kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kulinda amani ya nchi. SOMA: Tusipoamka tutaendelea kushangilia mafanikio ya kina Pacome