WAZIRI Mkuu, Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ya shule nchini ili kuhakikisha inakuwa rafiki kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni jijini Dodoma, Dk. Nchemba amesema hadi sasa Serikali imefanikiwa kujenga zaidi ya shule 7,600 jumuishi zenye miundombinu inayokidhi mahitaji ya wanafunzi hao kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari.

Ameeleza kuwa juhudi hizo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuhakikisha usawa katika upatikanaji wa elimu kwa makundi yote ya wanafunzi nchini.Kuhusu utekelezaji wa sera ya elimu bila malipo, Dk. Nchemba amesisitiza kuwa ni marufuku kwa shule kutoza fedha zisizo za lazima kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya baadhi ya maeneo, Waziri Mkuu amezielekeza ofisi zote za halmashauri kuanzia ngazi ya vijiji hadi mijini kusimamia kwa karibu suala hilo ili kudhibiti utozwaji wa fedha kinyume na sera ya elimu bure ya Serikali.SOMA: Shule jumuishi ya mfano yazinduliwa Mtwara

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *