
MBUNGE wa Jimbo la Ikungi Kaskazini Elibariki Kingu amesema Serikali imechukua hatua za makusudi za kuhakikisha taifa linabaki salama katika upatikanaji wa mafuta. Akichangia hotuba ya makadirio na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2026/2027 mjini Dodoma,Kingu amesema Serikali inatakiwa iweke mikakati endelevu ya kupunguza mzigo mkubwa wa kwa watanzania hasa katika kipindi hiki cha matatizo ya mafuta.
Hatahivyo, Kingu ameipongeza Serikali kwa kuchukua hatua za dharura za upatikanaji wa mafuta nchini. “Nawapongeza TPDC kwa hatua nzuri walizozifanya za kuweza kuhakikisha tunapata mafuta ya mwezi wa tano mpaka mwezi wa saba kwa kutoa maelekezo meli zishushe mafuta nchini,”alisema Kingu.
Katika mchango wake, Kingu ameiomba Serikali ijenge kituo cha kuhifadhia mafuta (storage facility) ambazo zitasaidia wakati wa dharura kwa lengo la kutumia na kuyauza katika nchi jirani pamoja na nchi nyingine zinazotuzunguka.
Pia amemuomba Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba akate matumizi ambayo hayana ulazima kuanzia mwezi wa nne mpaka wa mwezi wa saba ili fedha zitakazopatikana ziwekwe ruzuku kwenye mafuta ili yashuke bei na kuharakisha uchumi wa taifa.SOMA: Serikali yaahidi suluhisho kupanda mafuta