DAR ES SALAAM: MWANAMITINDO nguli Mtanzania, Miriam Odemba ameiomba Serikali kujizatiti kuunga mkono tasnia ya mitindo kwani inabeba sekta nyingi ikiwemo utalii.

Miriam Odemba ametoa ombi hilo katika tukio maalumu la mitindo ‘Muda Tanzanite Gala’ lililowakutanisha wanamitindo mbalimbali Dar es Salaam jana.

Akizungumza katika tukio hilo, Miriam ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema wanamitindo wengi wanapata nafasi kwenda mataifa ya nje hivyo, wanabeba na kuonesha utamaduni wa nchi.

“Kwa pamoja tunaweza kuisimamisha na kuipeleka mbele tasnia yetu, peke yangu siwezi, lakini kwa umona wetu inawezekana,” alisema Miriam.

Alisema kuwa kwa miaka mingi amejifunza kuwa mitindo si mavazi tu, bali ni utambulisho na pia ni nguvu ya kujieleza.

“Nawahimiza wote kuendelea kusimama imara, kuendelea kuamini vipaji vyenu, endeleeni kupeleka mbele tasnia,” ameongeza Miriam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *