
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, ameipongeza Benki ya CRDB kwa mchango wake mkubwa katika kuwainua wajasiriamali nchini kupitia utoaji wa elimu ya fedha na fursa za mitaji, hatua inayosaidia kukuza uchumi jumuishi na endelevu.
Akizungumza katika hafla ya Kitchen Party Gala 2026 iliyofanyika jijini Dar-es-salaam, Waziri Kapinga amesema ushirikiano kati ya sekta ya fedha na wajasiriamali ni muhimu katika kupunguza umasikini na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi, huku akisisitiza kuwa wanawake wana nafasi kubwa katika ustawi wa familia na taifa.SOMA: Mwongozo uwezeshaji wanawake wazinduliwa
Kwa upande wake, Benki ya CRDB imeendelea kujikita katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wachanga kupitia bidhaa na huduma za kifedha zinazolenga kuongeza ujuzi, mitaji na uwezo wa ushindani sokoni, sambamba na kusisitiza nidhamu ya matumizi ya fedha kwa maendeleo endelevu.
