#HABARI: Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 mkoani Dar es Salaam zinatarajiwa kuingia wilayani Kinondoni Aprili 17, 2026, ambapo utakimbizwa kwa umbali wa kilometa 63.9.

Katika mbio hizo, Mwenge wa Uhuru utakagua, utaweka mawe ya msingi, na kuzindua jumla ya miradi saba ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 9.2, ikilenga kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi kwa wakazi wa wilaya hiyo.

Viongozi wa Wilaya ya Kinondoni wamejipanga kuupokea Mwenge huo ambao ni alama ya umoja na uzalendo, wakisisitiza kuwa miradi itakayopitiwa inagusa sekta muhimu ikiwemo elimu, afya, na miundombinu ya barabara.

Wananchi wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru na kushuhudia matunda ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika kuwaletea maendeleo endelevu na kuimarisha ustawi wa jamii.

Powered by #MCHEZOSUPA

‎JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
‎-
‎Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

‎#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
‎Follow @itvtz @radioonetanzania
‎@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *