Côte d’Ivoire ilifuta visa vya forodha na Mali na Burkina Faso mnamo Aprili 11. Urahisishaji huu wa taratibu za usafiri ni muhimu kwa ajili ya kuongeza biashara na nchi jirani zinazotegemea sana uagizaji. Haya ni maendeleo muhimu kwa biashara.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hii inaashiria kuanguka kwa “Ukuta wa Berlin” wa kiutawala Afrika Magharibi, anasema mtaalamu katika masuala ya vifaa kutoka Côte d’Ivoire. Hatua hii itaokoa muda kwa wasafirishaji, hasa wanapovuka vituo vya mpaka kaskazini mwa Côte d’Ivoire huko Laléraba kwa Burkina Faso na Pogo kwa Mali.

Utekelezaji wa usindikaji wa hati za kielektroniki utaharakisha mchakato, anabaiisha Daouda Bamba, Katibu Mkuu wa chama cha Madereva wa Malori Afrika Magharibi, akizungumza na Alexis Bédu: “Inatufanya kuokoa muda.” Ili kwenda Mali au Burkina Faso, lori, ambalo limepakiwa katika bandari ya Abidjan, kwa mfano, linapaswa kuwa na hati za forodha. Kwa hivyo mara nyingi hilo huchukua muda mrefu sana: wiki moja, wiki mbili.”

Bila visa za forodha, gharama za vifaa hupunguzwa, kama vile ada za maegesho au hongo zinazohitajika wakati mwingine katika vituo vya ukaguzi.

Hii ni hatua muhimu, anakiri Youssouf Sangaré, mshauri katika masula ya vifaa huko Abidjan: “Itapunguza sana gharama ya bidhaa. Safari ambayo inatakiwa kuchukua siku moja au mbili kwa kiasi kikubwa itachukua tano. Gharama ya vifaa vya usafiri hupungua. Kuhusu gharama, kutakuwa na gharama ndogo zaidi ya kulipa.”

Côte d’Ivoire, Mali, na Burkina Faso pia wanaona hii kama njia ya kuongeza biashara yao. Hii inapaswa kuboresha ushindani wa bidhaa za ndani. Kulingana na mamlaka ya Côte d’Ivoire, kuondoa visa kunapaswa kupunguza muda wa kusubiri mipakani kwa saa 24 hadi 48.

Mnamo 2024, Mali ilithibitisha jukumu lake kama soko kubwa la Cote d’Ivoire, ikiwa ya tatu miongoni mwa wateja wa nchi hiyo ikiwa na karibu 8% ya mauzo ya nje ya Côte d’Ivoire, au takriban dola bilioni 1.5. Sehemu kubwa ya mauzo haya yanategemea bidhaa za petroli, ambazo zinasalia kuwa sehemu kuu ya biashara ya pande mbili.

Hata hivyo, uhusiano wa kibiashara na Burkina Faso unaonyeshwa na usawa mkubwa kwa upande wa Abidjan. Côte d’Ivoire ilisafirisha takriban bidhaa zenye thamani ya dola milioni 800 kwenda Burkina Faso mnamo mwaka 2024, ikilinganishwa na takriban dola milioni 170 katika uagizaji. Mtiririko wa biashara unatawaliwa na mafuta ya petroli yaliyosafishwa, tumbaku, na mafuta ya mawese upande wa Côte d’Ivoire, huku Burkina Faso ikisafirisha nje zaidi pamba mbichi na bidhaa za kilimo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *