Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi ametangaza Ijumaa alasiri kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz kwa meli za kibiashara. Uamuzi huu, uliokaribishwa na Donald Trump, pia umesababisha kushuka kwa bei ya mafuta.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, Abbas Araghchi ametangaza kuwa mlango bahari wa Hormuz uko wazi kwa muda ulio salia wa usitishaji mapigano.

Katika taarifa aliyochapisha kwenye mtandao wa X, Waziri wa Mamb ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, aliandika kuwa, “kulingana na usitishwaji wa mapigano nchini Lebanon, njia ya kupita kwa meli zote za kibiashara (mlango bahari wa Hormuz) uko wazi kwa kipindi kilichosalia cha usitishwaji mapigano, kwa njia zilizoratibiwa kama ilivyotangazwa na Shirika la Bandari na Usafiri wa Baharini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.”

Licha ya tangazo hilo Trump amesema kuwa vizuizi vya kijeshi vya Marekani katika bandari za Iran vitaendelea kuwepo hadi makubaliano ya amani na Tehran yatakapopatikana.

Mlango Bahari huo umefunguliwa saa kadhaa baada ya utekelezaji wa makubaliano ya kusimamisha mapigano kati ya Israel na Lebanon ulioanza Ijumaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *