#MAREKANI: Mtu mmoja amewaua watoto wake saba pamoja na mtoto mwingine ambaye si wa familia hiyo katika tukio la mauaji ya risasi yaliyotokea Shreveport katika Jimbo la Louisiana nchini Marekani, ambalo polisi wameelezea tukio hilo kama “mzozo wa kifamilia”.

Watoto hao walikuwa na umri wa kati ya mwaka 1 hadi miaka 14, kwa mujibu na shirika la habari la CBS.

Maafisa walisema tukio la risasi lilianza karibu saa 05:00 asubuhi (10:00 GMT) siku ya Jumapili. Mshukiwa alipiga risasi watu 10 kabla ya kukimbia kwa kutumia gari lililoibiwa, alisema msemaji wa Polisi wa Shreveport, Chris Bordelon.

Polisi walimfukuza na hatimaye kumuua.

Wanawake wawili watu wazima, wakiwemo mama wa watoto hao, wako katika hali mahututi hospitalini.

Mshukiwa ametambuliwa kama Shamar Elkins, kulingana na mkurugenzi wa mawasiliano wa meya wa Shreveport, Leigh Anne Evensky.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *