Mtu mwenye bunduki amewaua watoto wanane kwa risasi, tukio lililohusishwa na vurugu za nyumbani katika nyumba mbili tofauti mapema siku ya Jumapili asubuhi, Aprili 19, Shreveport, Louisiana, polisi imesema. Lilikuwa tukio baya zaidi la mauaji ya watu wengi nchini katika zaidi ya miaka miwili.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Hili ni tukio la kiwango kisicho cha kawaida kwa wengi wetu,” alisema Chris Bordelon, msemaji wa Polisi ya Shreveport. Waathiriwa walikuwa na umri wa kuanzia mwaka mmoja hadi 14, msemaji huyo wa polisi alisema, na baadhi walikuwa watoto wa mshukiwa. Jumla ya watu 10 walijeruhiwa kwa risasi.

Mshambuliaji alifariki baada ya kukabiliana na maafisa wa polisi waliomfyatulia risasi. Mshukiwa alijaribu kukimbia kwa gari na akafuatiliwa na polisi. Polisi hawakutoa jina lake lakini walisema alikuwa mwanaume mtu mzima. Mamlaka imebainisha kuwa bado walikuwa wakikusanya taarifa kutoka kwa matukio ya uhalifu kusini mwa jiji la Shreveport. Kulingana na ripoti za awali, mauaji hayo yalitokea baada ya mzozo wa kifamilia.

Polisi washangazwa na matukio

“Sina la kusema, nimepigwa na butwaa kabisa,” alisema Mkuu wa Polisi wa Shreveport Wayne Smith wakati wa mkutano na waandishi wa habari. “Siwezi kufikiria jinsi tukio kama hilo lingeweza kutokea.” “Hii ni hali ya kusikitisha, labda mbaya zaidi ambayo tumewahi kuipitia,” alisema Tom Arceneaux, meya wa jiji la kaskazini magharibi mwa Louisiana lenye wakazi wapatao 180,000.

Gavana wa Louisiana Jeff Landry alisema katika taarifa kwamba yeye na mkewe walishtuka sana. “Tunawashukuru sana maafisa wa polisi na wahudumu wa kwanza wanaofanya kazi bila kuchoka katika eneo la tukio,” aliongeza.

Vifo vingi kutokana na vurugu za silaha tangu mwaka 2024

Kulingana na data kutoka kwa shirika lisilo la kiserikali, Gun Violence Archive, hii ndiyo idadi mbaya zaidi ya vifo kutokana na vurugu za silaha nchini Marekani tangu vifo vya watu wanane katika kitongoji cha Chicago mnamo mwezi Januari 2024. Vurugu za sulaha ni janga linalojirudia ambalo serikali zilizofuata zimeshindwa kulidhibiti hadi sasa, kwani Wamarekani wengi bado wanamiliki silaha.

Kufikia mwaka wa 2025, karibu watu 15,000, bila kuhesabu watu waliojiua, watakuwa wameuawa kwa silaha za moto, kulingana na Gun Violence Archive.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *