Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa nchi yake haitaondoa kizuizi ilichoweka kwenye bandari za Iran hadi pale makubaliano rasmi yatakapofikiwa na Tehran.

Kauli hiyo imekuja wakati ambapo bado kuna sintofahamu kuhusu uwezekano wa kufanyika kwa mazungumzo mapya ya kumaliza vita kati ya pande hizo mbili.

Kizuizi hicho, ambacho kilianza wiki moja iliyopita, “kinaiangamiza Iran kabisa”, Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii wa Truth Social, akiongeza kuwa nchi yake ilikuwa ikishinda mzozo huo “kwa kiasi kikubwa”.

Maoni yake yanaambatana na makubaliano ya muda ya kusitisha mapigano kati ya Marekani na Iran yanayotarajiwa kukamilika Jumatano, lakini bado hakuna uhakika ikiwa awamu ya pili ya mazungumzo ya amani itaendelea nchini Pakistan.

Usalama umeimarishwa katika mji mkuu wa Pakistan kufuatia mkutano huo. Hata hivyo makamu wa rais wa Marekani JD Vance anayetarajiwa kuongoza ujumbe wa Marekani bado hajaondoka Washington, huku Iran ikisema bado haijaamua kuhudhuria.
#chanzobbcswahili

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *