#HABARI: Pakistan inaendelea na maandalizi ya mazungumzo ya kusitisha Vita baina ya Marekani na Iran, huku taarifa zikieleza kuwa Makamu wa rais wa Marekani JD Vance atasafiri siku ya Jumanne kuelekea Islamabad kuhudhuria mazungumzo hayo ikiwa yatafanyika.
Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuishambulia vikali Iran ikiwa haitafikia makubaliano mapya, huku Spika wa Bunge la Iran Mohammad Bagher Khalibaf akitaja kuwa wamejiandaa vilivyo na wako tayari kuonesha mbinu mpya kwenye uwanja wa vita.
Hayo yanajiri wakati makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki mbili yaliyoanza kutekelezwa Aprili 8, yanatarajiwa kufikia tamati usiku wa leo, hali inayozusha hofu ya kuzuka tena kwa vita hivyo vya Mashariki ya Kati.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)