
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, makubaliano ya kusitisha vita kati ya waasi wa M23/AFC licha ya kutiwa saini, bado hayatekelezwe kufuatia kuendelea kushuhudiwa kwa mapigano ya mara kwa mara.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wataalam wanaofuatilia mzozo wa Mashariki mwa DRC, wanasema, serikali ya Kinshasa na waasi wa M23/AFC wanapaswa kuanza kushirikiana pamoja ili kuhakikisha kuwa kilichokubaliwa kinafanyiwa kazi.
Kazi kubwa iliyo mbele ya pande hizo mbili ni kufuatilia, kuhakiki na kuchunguza ukiukwaji wowote wa mkataba huo na kuchukua hatua zitakazosaidia, kuheshimiwa kwa mkataba wa amani.
Wiki iliyopita, kwenye awamu nyingine ya mazungumzo nchini Uswizi, ilikubaliwa kuundwa kwa tume ya pamoja ili kufuatilia mchakato wa mazungumzo ya Doha na ule wa nchi za eneo la Maziwa Makuu ICGLR.
Wajumbe pia kutoka Marekani, Umoja wa Afrika watashiriki pia kama waangalizi kuona mwenendo wa utekelezwaji wa mkataba huo wa kusitisha vita kwenye mikoa ya Kivu Kusini na Kaskazini, na matokeo yatawasilishwa kwa wasuluhishi kwa mchakato wa Doha.
Haya yanajiri kufuatia mapigano mapya yaliyoripotiwa katika wilaya ya Minembwe, Kivu Kusini, ambapo jeshi la DRC limekuwa likitumia ndege zisizokuwa na rubani kuwalenga waasi wa M23/AFC.