Jeshi la wanamaji la kulinda mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, limesema, limekamata meli mbili, wanazosema zilkuwa zinafanya kazi bila idhini katika mlango wa Bahari wa Hormuz.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya jeshi la Iran imekuja, huku rais wa Marekani Donald Trump, akiongeza muda wa usitishwaji vita, ili kutoa fursa kwa Tehran kupendekeza namna inavyotaka mazungumzo yaendelee.

Iran inasema, jeshi lake linafuatilia kwa makini shughuli  zote zinazoendelea katika mlango huo wa Hormuz ambao wiki iliyopita, Marekani nayo ilizuia kupita kwa meli za Iran, kuishinikiza kukubali mkataba wa amani, hasa suala la kuachana kabisa na mradi wa nyuklia.

Rais Trump, amesisitiza kuwa bandari na meli za Iran zitaendelea kuzuiwa hadi pale mkataba wa amani utakapopatikana.

Naye Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi, amesema kuendelea kuzuiwa kwa meli za nchi yake, ukiukwaji wa mkataba wa usitishwaji vita.

Aidha, Iran imeitaka Marekani kuiondolea vikwazo vya kiuchumi, kufidia hasara zilizosababishwa na vita, na kuachia mali zake inazozuia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *