#HABARI: Baadhi ya wafanyabiashara wa viazi vitamu katika Soko la Mabibo jijini Dar es Salaam, wameuomba uongozi wa Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kutengeneza mfumo utakaowazuia wakulima kujaza viazi kinyume cha sheria yaani mfumo wa Lumbesa ili waweze kupata ushindani sawa katika biashara.
Mwenyekiti wa soko hilo, Yusuf Abdallah amesema changamoto kubwa ni baadhi ya maafisa wanawakamata wafanyabiashara na mizigo iliyojazwa kupitiliza katika soko hilo badala ya kuidhibiti mizigo iliyokiuka sheria katika maeneo ya uzalishaji wa viazi.
Nao baadhi ya wafanyabiashara wamesema wakulima katika mikoa inayozalisha viazi wamekuwa wakiwauzia wafanyabiashara mizigo iliyofungwa kwa lumbesa na hawako tayari kuwauzia wanaowajibika kununua kwa mujibu wa sheria.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)