‎#HABARI: Wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Sekondari Msangano, iliyopo kitongoji cha Sayuni, Kata ya Msangano, Wilaya ya Momba mkoani Songwe, wapo katika hatari ya kukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mimba za utotoni.

Hali hii inachangiwa na wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda na kurudi shuleni kutokana na ukosefu wa mabweni.

‎Wakizungumza kwa nyakati tofauti na ITV, katika mwendelezo wa maadhimisho ya Juma la Elimu yanayofanyika mkoani Songwe, baadhi ya wazazi na walezi wameeleza wasiwasi wao kuhusu usalama wa watoto wao pamoja na athari za hali hiyo kwa maendeleo ya elimu.

‎Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Msangano, Bi. Flora Kawonga, ameeleza changamoto zinazoikabili shule hiyo na mikakati wanayojaribu kuitekeleza ili kupunguza athari kwa wanafunzi, licha ya rasilimali kuwa chache.

‎Kwa upande wake, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala, akizungumza na wanafunzi, walimu pamoja na viongozi wa kitongoji hicho, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya jamii, Serikali na wadau wa elimu katika kuhakikisha mazingira salama na rafiki kwa wanafunzi yanapatikana, ikiwemo ujenzi wa mabweni.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *