Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar zimesaini mkataba maalum wa kushirikiana katika utekelezaji wa miradi ya elimu itakayohusisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia katika shule 20 za sekondari visiwani Unguja na Pemba.

Wakizungumza baada ya kusainiwa kwa mkataba huo Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha alisema, jukumu kuu la mamlaka hiyo ni kutafuta rasilimali fedha na vifaa kutoka kwa wadau wa maendeleo ya sekta ya elimu ili kuboresha miundombinu ya elimu nchini huku Naibu Katibu Mkuu (Taaluma) Dkt. Mwanakhamis Ameir licha ya juhudi zinazofanywa na Serikali, bado kuna changamoto kubwa katika sekta hiyo hivyo ushirikiano huo ni muhimu katika kuzitatua..

Dkt Kipesha ameongeza kuwa tayari fedha zimepatikana kupitia wadau hao likiwemo UNICEF na kusisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa awali na Mkurugenzi wa Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi ya Elimu wa TEA, Masozi Nyirenda, TEA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu katika visiwa vya Unguja na Pemba ambapo awali takribani Shilingi bilioni 3.2 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule za amali, huku bilioni 2.5 zikielekezwa katika ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo na maabara za sayansi katika shule 20.

Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *