Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani (Tumbi) imeipongeza Kampuni ya GFA Kibaha kwa uamuzi wake wa kuadhimisha miaka 19 tangu kuanzishwa kwake kwa kutoa msaada wa vitendea kazi, hatua itakayochochea utoaji wa huduma bora zaidi kwa jamii.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Aprili 24/ 2026, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Silas Msangi amesema vifaa vilivyotolewa ambavyo ni kompyuta nne (4) pamoja na matanki ya kuhifadhia taka, vitasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji wa kila siku hospitalini hapo.
Awali, akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Meneja wa Kiwanda cha GFA Kibaha, Ezra Merei, amebainisha kuwa kampuni hiyo inatambua kuwa afya ndiyo muhimili mkuu wa uchumi.
Alieleza kuwa licha ya shughuli zao za msingi kuwa ni uunganishaji wa magari, hawawezi kutenganisha uzalishaji na ustawi wa jamii inayowazunguka.
Maadhimisho hayo ya miaka 19 ya GFA yameleta tija ya kipekee mkoani Pwani, yakionyesha namna viwanda vinavyoweza kuwa chachu ya mabadiliko ya kijamii nje ya milango ya ofisi zao.
(Feed generated with FetchRSS)