Nchini Chad karibia watu 42 wameuwawa  baada ya makabiliano na mapigano kuzuka  Jumapili  kati ya makabila  yanayoishi mashariki mwa nchi hiyo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti  ya Mjumbe wa serikali  aliyefika eneo hilo  mapigano hayo yalianza kufuatia mzozo wa kisima kimoja  katika kijiji  kidogo cha Guereda kilichoko jimbo la Wadi Fira Mashariki mwa nchi hiyo.

Kufuatia hali hiyo mbaya ya kiusalama, Mawaziri kadhaa, maafisa wakuu wa eneo hilo, na mkuu wa majeshi walitumwa kwenye eneo la tukio kutathmini hali ilivyo.

Limane Mahamat Naibu Waziri Mkuu anayesimamia Utawala wa wilaya na ugatuzi, kwenye taarifa yake kwa kituo cha utangazaji cha serikali alisema, hali hiyo imedhibitiwa kwa sasa na utumivu umerejea

Kwa miaka kadhaa, eneo la mashariki mwa Chad limekuwa likikumbwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji  wa Kiarabu. Mvutano huo ukizidishwa  na wakimbizi wanaokimbia mapigano katika nchi jirani ya Sudan.

Migogoro hiyo  kuhusu mashamba na malisho ya mifugo imesababisha vifo vya zaidi ya elfu moja na  wengine  2,000 kujeruhiwa  kati ya mwaka wa 2021 na mwaka wa  2024, kulingana na ripoti  ya Shirika lisilo la Kiserikali la International Crisis Group.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *