#MuunganoCup “Kila mchezaji anajua umuhimu wa mchezo wa kesho, tuko tayari kupambana ili tuchukue taji”
Kiungo wa Simba SC, Semfuko Daud, amesema wachezaji wote wa timu hiyo wana ari na morali ya juu kuelekea fainali ya Kombe la Muungano dhidi ya Yanga.
Semfuko amesema wote wanatambua kuwa hakuna fainali zaidi ya hii, hivyo wako tayari kupambana na hawana presha yoyote.
“Presha siyo kubwa kwa kuwa kuna wachezaji wazoefu na wengi walishacheza mechi za aina hii”
Amewatoa hofu mashabiki wenye hofu na kiwango cha timu yao kwamba:-
“Tumejiandaa vizuri, hofu ya mashabiki wetu sisi ndiyo wa kuiondoa…”
Fainali ni Yanga vs Simba , Aprili 29, 2026.
#MuunganoCup2026 #KombeLaMuungano #SokaLinatuunganisha

(Feed generated with FetchRSS)