Nchini Cameroon, bado hakuna taarifa rasmi kutoka kwa mamlaka za ndani au viongozi kutoka serikali kuu kuhusu vurugu mbaya zilizotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Kaskazini Magharibi linalozungumza Kiingereza. Kulingana na RFI, angalau watu 14 walifariki katika vurugu hizo. Ukosefu wa uwazi kuhusu matukio hayo unasababisha wasiwasi miongoni mwa mashirika ya kiraia.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Angalau watu 14, wakiwemo wanawake, waliuawa katika kijiji cha Ndzerem-Nyam, katika tarafa ya Jakiri, katika jimbo la Bui, Kaskazini Magharibi mwa Cameroon. Vurugu hizi mbaya zilitokea wakati wa tukio la kitamaduni lililoandaliwa na jamii ya wenyeji. Pikipiki na majengo pia yanaripotiwa kuchomwa moto wakati wa shambulio hilo.

Lakini maelezo kuhusu mauaji haya yanatofautiana, na meni yanapingana, wakati mwingine yakiashiria mzozo kati ya jamii, au operesheni ya kijeshi iliyofanywa na vikosi vya serikali ya Cameroon kama sehemu ya mapambano dhidi ya makundi yenye silaha yanayotaka kujitenga katika maeneo yanayozungumza Kiingereza.

Waathiriwa ni akina nani? Raia au wanaotaka kujitenga, na ni akina nani waliohusika na shambulio hili baya? Viongozi w Cameroon hawajazungumza chohote.

Chini ya siku 10 baada ya ziara ya Papa huko Bamenda

Mauaji haya yanakuja chini ya siku kumi baada ya ziara ya Papa Leo XIV huko Bamenda, mji mkuu wa eneo la Kaskazini Magharibi, ambalo limekumbwa na vurugu kwa zaidi ya miaka minane.

Kufuatia ziara hii, mashirika kumi na mawili ya kiraia ynchini Cameroon yalitoa wito wa pamoja wa kufunguliwa mara moja kwa mazungumzo jumuishi ili kukomesha mgogoro na vurugu ambazo zimekuwa “za kawaida” na zisizoadhibiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *