KAMPUNI kinara ya Mawasiliano nchini ya Yas Tanzania, inajivunia mapinduzi chanya ya kidijitali na mafanikio iliyoyapata katika kipindi cha mwaka mmoja wa chapa hiyo, ambayo imekuwa ni sio tu mtandao wa mawasiliano, bali jukwaa huru linalowaunganisha Watanzania na fursa za kiuchumi, kijamii na kiteknolojia.

 Mafanikio hayo yametokana na uwekezaji mkubwa wa miundombinu, ubunifu wa huduma na upanuzi wa kimfumo, ikiimarisha mtandao wake wa 4G na 5G, ambapo imetumia zaidi ya Sh. Trilioni 1 kugharamia miradi ya upanuzi wa miundombinu kukidhi mahitaji ya wateja wake Tanzania bara na visiwani.

Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Yas, Pierre Canton-Bacara, wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa makala haya, ambapo aliitaja Yas kuwa ndio mtandao wa viwango Tanzania, utambulisho mpya unaoakisi uwekezaji wa muda mrefu uliofanywa na kampuni hiyo ili kuboresha miundombinu yake inayojumuisha minara mingi.

Katika mahojiano hayo Pierre ikCanton-Bacara alibainisha kuwa, upanuzi wa mtandao umesaidia kuhudumia vema  wateja wao zaidi ya milioni 30, hivyo kuongeza ubora wa huduma kupitia intaneti yenye kasi inayoifanya Yas kuwa mtoa huduma za kidijitali anayeaminika zaidi katika dunia ya hii ya sayansi na teknolojia.

Akieleza ni kwa nini Yas umekuwa Mtandao wa Viwango, Canton-Baacara alisema Uwekezaji mkubwa walioufanya na upatikanaji wa huduma zao bora, ndio unaowapa uhalali wa kutumia utambulisho huo, ikiwemo upatikanaji wa mtandao unaotokana na wingi wa minara kuliko kampuni yoyote ya mawasiliano Tanzania. 

“Tuna minara ya mawasiliano 4,800+ ambayo ni takribani minara 1,000 zaidi kuliko mtandao mwingine wowote Tanzania, huku mtandao wetu ukiwa na kasi inayomstahili mtumiaji katika kukamilisha malengo yake, kama ilivyothibitishwa wataalamu wa ndani na nje ya nchi, ikiwemo Taasisi ya Ookla.

“Kwa mwaka wa tatu sasa, taasisi hiyo imeitambua na kuthibitisha kuwa Yas ndio mtandao wenye kasi zaidi Tanzania kupitia vipimo vya speedtest, utambuzi ambao sio tu unawahakikishia watumiaji wetu nguvu ya kufurahia ufanisi wa kihuduma, bali utimilifu wa ndoto nyingi za Watanzania popote watumiapo mtandao wetu,” alisema.

“Leo hii kuna mkulima kule Shinyanga anapata taarifa za soko, kuna mfanyabiashara kule Mbeya nauza mazai yake mtandaoni, kuna mwanafunzi anasoma chuo cha nje,  vijana leo hii wanajipatia kipato kupitia mtandao, kuna madaktari wanatoa elimu ya afya mtandaoni. nzania. Mtandao bora na wa uhakika unafungua fursa ambazo zinaleta matokeo chanya kwenye maisha ya watanzania. 

Akizungumzia ushindani wa Sekta ya Mawasiliano, siri ya mafanikio yao na kile kinachoutofautisha Yas na mitandao mingine, Canton-Bacara, alisema mambo matatu yameiweka kampuni hiyo katika ‘dunia ya peke yao’ kihuduma, akiyataja kuwa ni uimara wa mtandao, upana wa huduma zao za kidijitali, na dhamira ya ujumuishi.

Alifafanua kuwa, kwenye uimara na upana wa mtandao, Yas wanaendelea kupanua mtandao wa 4G na 5G pamoja na huduma za intaneti, jambo linalowezesha kasi kubwa ya intaneti, hivyo huduma kufika katika maeneo mengi, na kuwa na mtandao wenye uhakika zaidi Tanzania.  

Bacara alieleza kuwa  Pamoja na kuhakikisha wanakuwa na mtandao wa viwango unapoatikana kila mahalai, kampuni hyo pia imejikita katika kuhakikisha upatikanaji wa zana za kidijitali, hususan simu janja. Kupitia simu za mikopo na ofa zinginezo wameweza kuongeza matumizi ya simu  njanja kwa asilimia 17 toka mwaka jana.

“Hii imefungua milango kwa Watanzania wengi zaidi kupata huduma za kidijitali na kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi, lakini pia tumewekeza katika programu za uwezeshaji wa kidijitali zinazomlenga mwananchi moja kwa moja, mfano hai ukiwa ni mradi kama ‘Apps and Girls’ na Programu ya E-School,” alisisitiza.

Alisema kuupitia upanuzi wa mtandao wa simu na intaneti, mamilioni ya Watanzania wameweza kuwasiliana kwa urahisi, kufanya biashara, kupata taarifa, na kuishi kisasa katika ulimwengu wa kidijitali.

 Aliongeza kuwa kasi ya mtandao ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kidijitali na kwamba Yas imeendeleza historia nzuri iliyodumu kwa zaidi ya miaka 30, na kuwa safari ya Yas imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa Taifa, ikiwemo kuunganisha Watanzania kupitia mawasiliano na kuwapatia fursa za kiuchumi.

 “Mwaka uliopita pekee, tulinunua bidhaa na huduma zenye thamani ya zaidi ya Sh569 bilioni kutoka kwa wazabuni wazawa, huku tukilipa Sh. Bilioni 418 kama Kamisheni kwa washirika wetu, na tulichangia zaidi ya Sh. Trilioni 2.8 kama Kodi kwa Serikali katika kipindi cha miaka mitano iliyopita,” alifafanua Canton-Bacara.

 Aidha, alisema Yas imekuwa ikiajiri mamia ya watanzania moja kwa moja na kutengeneza fursa za ujasiriamali kama vile mawakala zaidi ya 300,000 kote nchini kujipatia kipato, hivyo  kushiriki katika ukuaji wa Uchumi wa taifa. Lakini pia Yas inaendelea kuchangia ustawi wa jamii katika Sekta za Afya, Elimu, Uwezeshaji Kiuchumi na Uhifadhi wa Mazingira kupitia Programu zake kwa Jamii (CSR).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *