#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Bi. Victoria Mwanziva, leo Mei Mosi amepokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi, Bw. Hassani Ngoma Mei Mosi, 2026.

Bi. Victoria Mwanziva, amesema Mwenge huo wa Uhuru mwaka 2026 ukiwa katika Halshauri ya Mtama umetembelea miradi mitano, miradi 4 itawekwa mawe ya msingi na mradi mmoja utazinduliwa.

Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Kikundi cha Vijana Fahari group, umaliziaji wa madarasa 2 na ofisi shule la Msingi Mihongoni, Ujenzi wa Jengo la X-Ray Kituo cha Afya Mtama, Ujenzi wa Shule ya Wavulana Kanda Kiwalala (Lindi Boys) pamoja na Ujenzi wa Kiwanda cha Ubanguaji Korosho.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Lindi, amesema Miradi yote mitano inathamani ya shilingi Bilioni 5.4.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *