LICHA ya kuonekana kutofurahishwa na matokeo ya sare mfululizo, Kocha Mkuu wa Mashujaa Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amesema timu hiyo haishuki daraja na kama ikitokea anaachana na masuala ya mpira.

Hiyo ni mara ya tatu kwa kocha huyo kutoa kauli ya kuachana na mpira kwa misimu tofauti ambapo awali alikuwa akiinoa Mwadui FC iliyokuwa mkoani Shinyanga (kwa sasa Big Man), Dodoma Jiji na sasa ameirudia tena akiwa Mashujaa FC.

Julio amekabidhiwa timu hiyo takribani miezi miwili sasa ambapo ameiongoza Mashujaa michezo sita ikiwamo ya Kombe la Shirikisho, akishinda miwili na sare nne na kuwa nafasi ya 11 kwa pointi 22.

JULI 01

Mechi alizoongoza kocha huyo mwenye maneno mengi na kuambulia sare ni Tanzania Prisons, Fountain Gate, Azam na Mbeya City, huku akishinda dhidi ya Mtibwa Sugar na Geita Gold mchezo wa Kombe la Shirikisho kwa penalti 4-3 baada ya suluhu ya bila kufungana.

Akizungumza jijini Mbeya, Julio amesema timu hiyo bado ni nzuri japokuwa tatizo lipo katika kumalizia nafasi wanazopata kufunga mabao akiahidi kulifanyia kazi ili kuweka utulivu uwanjani.

Amesema pamoja na matokeo waliyonayo, anaamini Mashujaa haiwezi kushuka daraja akisisitiza kuwa iwapo itatokea atatangaza rasmi kustaafu, huku akieleza kuwa hataki kumlaumu mtu kwa yanayotokea uwanjani.

JULI 02

“Ukicheza ukapata ushindi au sare lazima ushukuru, mazongere ni mengi sana uwanjani, lakini bado timu yangu ni imara na ndio maana hatujapoteza mchezo, tatizo ni utulivu kwa wachezaji katika kufunga mabao kwenye nafasi tunazopata.

“Bado tuna mechi 10 zilizobaki, niseme Mashujaa haishuki daraja na nitangaze kabisa kama tutashuka daraja naachana na mpira kabisa, kwa kuwa nayajua mazingira ya mpira ndio maana bado nipo,” amesema Julio.

JULI 03

Kwa upande wake straika wa timu hiyo, Chrispin Ngushi amesema matokeo ya sare mfululizo si mazuri sana  lakini bado wanayo matumaini ya kufanya vizuri katika mechi zilizobaki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *