Nchini Mali, baada ya kuiteka Kidal mwihini mwa wiki iliyopita, wanajihadi wa kundi linalodai kuunga mkono Uislamu na Waislamu (JNIM) na waasi wanaotaka kujitenga wa Azawad Liberation Front (FLA) walichukua udhibiti wa kambi za kijeshi za Tessalit na Aguelhoc siku ya Ijumaa, Mei 1. Kusonga mbele kwao kunasababisha wasiwasi miongoni mwa wakazi wa miji mikubwa kaskazini mwa Mali.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa usiku wa Aprili 30 kuamkia Mei 1, JNIM inajaribu zaidi kuliko hapo awali kujiweka kama mdau wa kisiasa, ikitoa wito kwa “vikosi vyote muhimu vya taifa la Mali” kupindua utawala wa sasa. Mamlaka ya mpito bado imeazimia kupigana na kudumisha udhibiti wao madarakani, kwa usaidizi wa Urusi. Operesheni za kijeshi zinaendelea, na meli za mafuta zimeingia Bamako, licha ya kizuizi cha wanajihadi.

Seidane Ag Hitta, mmoja wa viongozi wakuu wa kundi linalodai kuunga mkono Uislamu na Waislamu (JNIM), anapiga picha kwa fahari katika kambi ya kijeshi ya Tessalit pamoja na Abdallah Ag Albaka, kiongozi mwingine wa kijeshi wa kundi hila wanajihadi. Mkononi mwake, anashikilia ufunguo wa kambi hiyo, ambayo ilikabidhiwa miaka mitano iliyopita kwa vikosi vya Mali kutoka kikosi cha Ufaransa cha Barkhane, ambacho baadaye kilifukuzwa kutoka Mali. Picha hiyo ilithibitishwa kwa RFI na vyanzo kadhaa vilivyohusika moja kwa moja. Kufuatia kujiondoa kwa wanajeshi wa Mali na washirika wao wa Urusi, Africa Corps, JNIM na wapiganaji wa Azawad Liberation Front (ALF) waliingia katika kambi hii na kambi ya Aguelhoc bila mapigano mnamo Mei 1.

Tangu kutekwa tena kwa Kidal mnamo Aprili 25, makundi hayo yenye silaha yalikuwa tayari yamerudi Ber, Tessalit (ambapo wanajeshi wa Mali walijisalimisha kwa njia ya mazungumzo), miji ya Hombori, na Gourma Rharous, ililengwa siku ya Ijumaa na shambulio la pili katika siku mbili.

Lengo linalofuata

JNIM na FLA ni wazi hawana nia ya kuacha kusonga mbele. “Hali ya mwaka 2012 inajitokeza,” kongozi mashuhuri huko Timbuktu. Wakati huo, miji mikuu ya Kaskazini ilianguka katika siku chache tu. “Unaweza kuhisi wasiwasi wa wanajeshi,” chanzo hiki kinaendelea. Huko Gao pia, wakazi wanaonekana kukabiliwa na hali ngumu: “Karibu maduka yote yamefungwa, hakuna kinachoendelea, tuko hapa tukitazama tu,” anaelezea mkazi mmoja. Watu wa maeneo ya kaskazini wanajiuliza kuhusu lengo linalofuata la makundi haya yenye silaha na wanajiandaa kwa mapigano zaidi.

Lakini mamlaka ya mpito na washirika wao wa Urusi wako mbali na kuweka silaha zao chini. Jiji la Kidal na viunga vyake yanashambuliwa kwa mabomu mara kwa mara. Jeshi la Mali lilibainisha katika taarifa kwamba lililenga ofisi ya gavana na kambi ya kijeshi ya jiji hilo mnamo Aprili 29, pamoja na ghala la silaha na vifaa. “Mashambulizi ni makubwa zaidi nje ya jiji kuliko ndani yake,” anashuhudia mpiganaji wa waasi aliyepo Kidal, ambaye anaelezea kwamba malengo ni magumu kutofautisha katika jiji kuliko jangwani, “ambapo kila gari chini ya mti linabaki hatarini.” Jeshi linadai “kuwaangamiza magaidi kadhaa” na kuharibu vifaa, dai linalopingwa na vyanzo kadhaa ndani ya FLA. Hakuna tathmini huru ya mashambulizi haya ambayo imethibitishwa.

Jeshi la Mali na washirika wake wa Urusi wamejiondoa hadi Anefis, nafasi ya mwisho ya kijeshi katika eneo la Kidal ambayo bado haijatekwa na makundi yenye silaha.

Operesheni za Africa Corps na kuwasili kwa malori ya mafuta

Kikosi cha wanamgambo wa Urusi wa Africa Corps, ambacho sasa kinatoa taarifa nyingi kwenye mitandao ya kijamii, pia kinadai kufanya operesheni katika siku za hivi karibuni katika maeneo ya Gao, Ménaka, Sikasso, na Koulikouro, kikisisitiza azimio lake la kuendelea na mapigano pamoja na jeshi la Mali.

Kufuatia makubaliano yaliyoruhusu wapiganaji wa Urusi kuondoka Kidal salama baada ya kushindwa kwao mwishoni mwa wiki iliyopita, mashaka yaliibuka kuhusu kuendelea kwao kupigana nchini Mali. Mnamo Aprili 30, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alihakikisha wazi kwamba Urusi “itaendelea kutoa msaada kwa mamlaka zilizoko madarakani” na itaendeleza “mapambano yake dhidi ya msimamo mkali, ugaidi, na dalili zingine mbaya.”

Huko Bamako, JNIM inatekeleza hatua kwa hatua kizuizi kilichotangazwa siku ya Jumanne ya wiki hii: vituo vya ukaguzi vimewekwa katika barabara kadhaa zinazounganisha mji mkuu na sehemu nyingine ya nchi, ambapo wanajihadi wanazuia magari katika pande zote mbili. Hata hivyo, kulingana na taarifa rasmi kutoka kwa serikali ya Mali na kikosi cha wanamgambo wa Urusi, Africa Corps, msafara wa malori zaidi ya 800 ya mafuta uliweza kuingia katika mji mkuu siku ya Ijumaa, wakati jeshi na washirika wake kutoka Urusi wakisindikiza msafara huo kwa njia ya ardhini na angani.

Siku ya Ijumaa, katika taarifa kwa vyombo vya habari, mwendesha mashtaka wa umma katika mahakama ya Bamako alitangaza kukamatwa kwa wanajeshi kadhaa wa Mali wanaoshutumiwa kushiriki katika mashambulizi ya siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *