
Mgogoro katika Mashariki ya Kati una athari kubwa duniani kote, na kuathiri vibaya minyororo ya usambazaji wa misaada ya kibinadamu duniani na utoaji wa misaada. Gharama za juu za usafiri na usumbufu wa mizigo vinasababisha Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) kurekebisha mkakati wake wa utoaji.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hali barani Afrika inatia wasiwasi hasa, kwani bara hilo linakabiliwa na migogoro mingi, ambayo mara nyingi hupuuzwa kulingana na UNHCR, na ambayo inasababisha watu kuhama makazi yao.
Ongezeko la bei ya mafuta la takriban 15% nchini Kenya, kunakopatikana moja ya vituo vikuu vya usambazaji vya kikanda vya shirika hilo la Umoja wa Mataifa, limesababisha ucheleweshaji wa utoaji wa misaada. Ucheleweshaji huu unazidishwa na kupungua kwa idadi ya malori yanayopatikana kwa ajili ya usafirishaji kwenda Ethiopia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na Sudan Kusini.
Kuongezeka maradufu kwa gharama za misaada
Kuhusu Sudan, ambayo inakabiliwa na mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani, gharama ya utoaji wa misaada imeongezeka maradufu katika miezi ya hivi karibuni, Unaonya Umoja wa Mataifa, hasa kwa vile usafirishaji huu unalazimika kuzunguka Afrika. Hii inaongeza siku 25 kwa muda wa uwasilishaji.
“Watu walio na uhitaji mkubwa wanapokea vifaa kwa kuchelewa ambako hakuonyeshi tena uharaka wa hali hiyo,” amesema Carlotta Wolf, msemaji wa UNHCR, kwa waandishi wa habari huko Geneva. Kwa baadhi ya usafirishaji, bei zimeongezeka zaidi ya mara mbili. Hii ndiyo hali ya kusafirisha vitu vya misaada kutoka ghala la UNHCR huko Dubai hadi Sudan na Chad. Gharama zimeongezeka kutoka dola 900,000 hadi dola milioni 1.87.
Vikwazo vya bajeti
Mgogoro huu na Iran “unawaathiri watu katika hali za dharura kwa kiasi kikubwa,” UNHCR inalalamika. Usumbufu huu unakuja wakati ambapo shirika hili la Umoja wa Mataifa linakabiliwa na vikwazo vikali vya bajeti kufuatia kupunguzwa kwa gharama kutoka kwa wafadhili wa kimataifa.