
Shirika la Habari la Fars limetangaza kuwa, meli ya Jeshi la Wanamaji la Marekani imepigwa kwa makombora mawili baada ya kupuuza onyo la Jeshi la Majini la Iran.
Meli hiyo, ambayo ilikuwa ikisafiri (Jumatatu) kinyume na usalama wa trafiki na urambazaji karibu na kisiwa cha Jask kwa nia ya kuvuka Lango Bahari la Hormuz, imeshambuliwa kwa makombora baada ya kupuuza onyo la Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Baada ya mashambulizi hayo meli hiyo ya kijeshi ya Marekani imelazimija kukatisha safari yake na kukimbia eneo hilo.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hapo awali ilikuwa imetangaza mara nyingi kwamba haiwezekani kupita Mlango Bahari wa Hormuz bila kupata ruhusa rasmi kutoka Iran na kwamba kupuuza onyo hilo kutakabiliwa na jibu la haraka kutoka kwa vikosi vya jeshi la ulinzi.